Zenj FM

Kamishna wa Polisi UN Asifu Utendaji wa Polisi Kamisheni ya Zanzibar

4 December 2024, 8:26 pm

Mkuu wa Polisi wa Umoja wa Mataifa Kamishna Faisal Shahkar, Akizungumza na Maafisa wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.

Na Omar Hassan.

Mkuu wa Polisi wa Umoja wa Mataifa Kamishna Faisal Shahkar amesema amefurahishwa na juhudi na umahiri wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamisheni ya Zanzibar katika kuzuwia uhalifu na kuifanya Zanzibar kuwa ni sehemu salama.

Akizungumza na Maafisa wa Polisi, Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kamishna Faisal amesifu Namna ya Jeshi hilo linavyoshirikiana na vyombo vyengine katika kukabiliana na makosa mbalimbali yakiwemo ya udhalilidhaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto.

Aidha ameeleza kuwa Umoja wa Mataifa upo tayari kulisaidia Jeshi la Polisi Tanzania kwa kuliwezesha katika Nyanja tofauti ili kufanikisha kuzuwia uhalifu.

Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad amesema ziara ya Kamishna huyo Visiwani Zanzibar ina dhamira ya kuimarisha umoja baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na umoja wa Mataifa katika kukuza Amani, usalama na maendeleo.

Amesema Tanzania inajivunia kuwa mshiriki hai katika juhudi za kulinda Amani za Umoja wa Mataifa kwani Polisi na Wanajeshi wanaendelea kutoa huduma ya ulinzi katika nchi tofauti duniani.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad.