Zenj FM

Makamanda wa mikoa Zanzibar watakiwa kupambana na wanyang’anyi

25 November 2024, 6:08 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad akizungumza alipokua akizindua opersheni maalum ya kukabiliana na uhalifu na ukikiukwaji wa sheria za barabarani.

Na Omary Hassan

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amewataka wananchi kuendelea kuitunza amani iliopo kwani ni kichocheo kikubwa cha utalii hapa nchini.

Ameyasema hayo huko katika shehia ya Kwamtipura alipokua akizindua opersheni maalum ya kukabiliana na uhalifu na ukikiukwaji wa sheria za barabarani amesema sekta ya utalii imekua ikilet maendeleo makubwa hapa nchini na inamgusa kila mmoja katika jamii hivyo endapo nchi itakapokua haina Amani itapelekea watalii kutokuja Zanzibar.

CP HAMAD amesema mtalii yoyote yule anapo chagua sehemu ya kwenda kutalii kwanza huangali usalama wake ndiomana Zanzibar imekua ikipokea wageni wengi kutokana na usalama uliopo hivyo amewataka wananchi kuitunza Amani iliopo ili wageni hao waendelee kuja.

Kwaupande mwengine amesema sekta ya Usafiri wa pikipiki(Boda boda) ni sekta muhimu sana ambapo wananchi hujiapatia kipato licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo wizi, mauaji ya madereva pikipiki na ukiukwaji wa sheria za barabarini, amaesma operesheni hio itaenda kutatua changamoto hizo na kuzuia na kukuabiliana na wahalifu huo.

Aidha amewaagiza Makamanda wa Mikoa yote mitano ya Zanzibar kushirikiana na wananchi kuhakikisha wanawashuhulikia kwa mujibu wa sheria bila ya huruma wahalifu wote wanao jihusisha na unyanganyi wa kutumia mapanga, wizi wa pikipiki kwa kufanya operesheni ya nyumba kwa nyumba.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Mchomvu amesema takribani watuhumiwa hamsini (50) walikamatwa kwenye Operesheni ya kuzuia mapanga iliyozinduliwa mwezi Mei 2024, wanatumikia adhabu za vifungo jela ambapo ameahidi kuendelea kusimamia operesheni hiyo ili kuhakikisha wahalifu wanadhibitiwa.

Sauti ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Mchomvu.