Zenj FM

CP Hamad awataka polisi kutomwonea mtu

15 November 2024, 4:38 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Hamad Khamis Hamad, Akifunga Mafunzo huko Chuo cha Polisi Zanzibar .

Na Omar Hassan

Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Hamad Khamis Hamad amewataka Askari waliohitimu mafunzo ya uongozi mdogo ngazi ya Sajent amewataka kufanya kazi kwa kutenda haki bila ya kumuonea au kumpendelea mtu.

Akifunga Mafunzo hayo huko Chuo cha Polisi Zanzibar Cp. Hamad amesisitiza kwa Askari wa Jeshi la Polisi kuwa na nidhamu na uadilifu katika utekelezaji wa majukumu yao.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Hamad Khamis Hamad,

Akitoa tathmini ya Mafunzo hayo Kozi namba 1/2024-2025 Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP MOSES NECKEMIAR FUNDI amesema mafunzo hayo yametolewa wakati muwafaka kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa nchi.

Sauti ya Mkuu wa Chuo cha Polisi Zanzibar Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Moses Neckemiar Fundi.

Jumla ya Askari 1,015 kutoka Mikoa yote ya Tanzania walihudhuria mafunzo hayo yaliyotolewa kwa muda wa wiki nane.