Kampeni ya Tuwaambie kabla hawajaharibiwa yazinduliwa Kusini Unguja
20 October 2024, 7:07 pm
Na Mary Julius.
Mkuu wa Wilaya ya Kati Sadifa Juma Khamis amezindua Kampeni ya Jeahi la Polisi Tanzania ya Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa na kulipongeza Jeshi la Polisi na Serikali kwa mikakati inayochukuwa katika kuhakikisha kaki za Watoto zinalindwa na kuheshimiwa.
Akizindua Kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja huko Tunguu Katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, Sadifa amesema Jeshi la Polisi na Serikali kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuwa mfano mzuri wa kuheshimu Mikataba ya Kimataifa katika kulinda haki za Binaadamu.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo Jamii, Jinsia na Watoto Siti Abasi Ali amesema serikali imeweka juhudi nyingi na mikakati mingi ili kuzuia vitendo vya udhalilishaji hivyo ameiomba jamii kuondosha muhari ili kuweza kuondosha vitendo hivyo.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Kamishna Msaidizi wa Polisi Acp. Khamisi Mwampwela amesema lengo la Kampeni ya Tuwaambie Kabla Hawajaharibiwa ni kuzuwia vitendo vya udhalilishaji.
Nae Mratibu wa Madawati ya Jinsia ya Vyuo vikuu Said Suleiman Ali ameeleza kuwa kampeni hiyo pia itasaidia kuzuwia udhalilishaji katika vyuo Vikuu kwa kuwa udhalilishaji upo katika vyuo na kwamba kwa kipindi cha wiki mbili wamepokea kesi tatu za udhalilishaji.