Zenj FM

Wanaokubali kuingiliwa klinyume na maumbile wana makosa

2 September 2024, 4:34 pm

Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamisheni ya Zanzibar Mkaguzi Msaidizi Sadik Ali Sultan akitoa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji huko Kinyasini Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini

Omar Hassan

Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamisheni ya Zanzibar Mkaguzi Msaidizi Sadik Ali Sultan amesema wanaokubali kuingiliwa kinyume na maumbile wana makosa kwa mujibu wa Sheria na wanastahiki kushtakiwa na hatimae kufungwa kutumia adhabu ya makosa yao.

Akitoa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji huko Kinyasini Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja Sadiki amesema hali hiyo inawaathiri zaidi baadhi ya wasichana wanaodaiwa kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile kukwepa kupata ujauzito, hivyo amewaasa kuacha tabia hiyo.

Sauti ya Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Tanzania Kamisheni ya Zanzibar Mkaguzi Msaidizi Sadik Ali Sultan.

Nae Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo ya Jamii na Huduma Zanzibar (JUMAJAHUZA) Ali Mohd Kassim amesema jumuiya hiyo inashirikiana na Jeshi la Polisi kuweka mikakati ya kuwasaidia Viongozi wa Nchi na Jamii kukomesha vitendo vya udhalilishaji nchini Tanzania.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jumuia ya Maendeleo ya Jamii na Huduma Zanzibar (JUMAJAHUZA) Ali Mohd Kassim.

Mapema akifungua Mafunzo hayo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kaskazini A Machano Fadhili Machano amehimiza ushirikiano katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya Watoto.

Sauti ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kaskazini A Machano Fadhili Machano.