Zenj FM

SMZ kulisaidia jeshi la polisi kukabiliana na uhalifu

26 August 2024, 6:16 pm

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma akizungumza na Maafisa wa Polisi Mahonda Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

OMar Hassan.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar italipa nguvu Jeshi la Polisi ili liweze kufanya kazi ya kulinda maisha ya watu na mali zao kwa ufanisi.

Akizungumza na Maafisa wa Polisi huko Mahonda Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja mara baada ya kufanya ziara kukagua Vituo vya Polisi vya mikoa mitatu ya Unguja yenye lengo la kuangalia changamoto ili zifanyiwe kazi Hamza ameliagiza Jeshi la Polisi kukabiliana na changamoto za uhalifu ukiwemo wa ajali zinazosababishwa na waendesha bodaboda, udhalilishaji na makosa dhidi ya raia wa kigeni.

Aidha amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaunga mkono Juhudi za Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wanaohatarisha Amani ya Nchi kwa kutoa maneno ya uchochezi na kuwahamasisha wananchi kufanya fujo.

Sauti ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raisi, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Raisi, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma (aliyevaa suti) akiwa katika ziara ya kukagua Vituo vya Polisi vya Mikoa mitatu ya Unguja.

Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad ameiomba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kulisaidia Jeshi la Polisi vyenzo za kufanyia kazi zikiwemo boti na kamera za Drone ili wananye doria katika sehemu za uwekezaji na utalii.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp. Hamad Khamis Hamad.