Zenj FM

Masheha toeni ushirikiano kwa jeshi la polisi

22 August 2024, 6:38 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Hamad Khamis Hamad akizungumza na masheha, Polisi Shehia pamoja na maafisa wa Polisi kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano Chuo cha Polisi Zanzibar.

Na Omar Hassan

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amewataka Masheha wa Mkoa wa Mjini Magharibi kuendelea kudumisha ushirikiano na Jeshi la Polisi ili kuzuia uhalifu katika maeneo yao.

Kamishna Hamad ametoa wito huo wakati akizungumza na masheha, Polisi Shehia pamoja na maafisa wa Polisi kwenye kikao kilichofanyika ukumbi wa mikutano Chuo cha Polisi Zanzibar.

Amesema kudumisha ushirikiano baina ya Polisi Shehia na Masheha itakuwa njia rahisi ya kubaini changamoto katika maeneo yao na kutafuta ufumbuzi wa pamoja ambao utaleta matokeo chanya kwa jamii.

Aidha, amewataka masheha kuwa mabalozi wa kufikisha ujumbe kwa wananchi kutambua umuhimu wa kufika na kutoa ushahidi mahakamani ili kuwatia hatiani watuhumiwa wa makosa mbalimbali.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar Cp Hamad Khamis Hamad.
Hamad Salum Ha,ad Sheha wa Munduli.

Nae Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharib Moh’d Ali Abdalla Amelipongeza Jeshi la
Polisi kwa hatua walioichukua kupitia dhana ya Polisi jamii kwa kua karibu na wananchi ili
kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarika.

Sauti ya Katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharib . Moh’d Ali Abdalla

Kwa upande wao Masheha wamesema changamoto kubwa inayopelekea kuendelea kwa
makosa katika jamii ni swala la muhali.

Sauti za masheha

Kikao hicho kimelenga kuboresha utendaji wa Polisi shehia na Masheha katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama.