Zenj FM

Wananchi watakiwa kuchangamkia fursa za kijamii zinazotolewa na polisi

22 August 2024, 2:37 pm

Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad akipokea vifaa tiba kutoka Jumuiya ya Korea Friend of Hope International wakishirikiana na Jumuiya ya kuboresha Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi Pemba (JUKUMAKIKIPE).

Na Omar Hassan.

Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar limekabidhiwa vifaa tiba pamoja na Jengo na vifaa kwa ajili ya Karakana ya Polisi Mikoa ya Pemba vyenye thamani ya T.Sh. milioni 85, kutoka kwa Jumuiya ya Korea Friend of Hope International wakishirikiana na Jumuiya ya kuboresha Maendeleo ya Jamii na Kiuchumi Pemba (JUKUMAKIKIPE).

Akipokea vifaa vivyo huko Kambi ya Polisi Madhungu Mkoa wa Kusini Pemba, Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad amesema Vifaa hivyo vitasidia kuimarisha Utendaji katika kuihudumia jamii na amewataka wananchi kuchangamkia fursa za huduma za kijamii zinazotolewa na Jeshi la Polisi ikiwemo huduma za Afya na Elimu.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad.

Mwakilishi wa Jumuiya ya Korea Friend of Hope International Ushindi Philipo Maiko amesema wameamua kutoa misaada hiyo kwa Jeshi la Polisi kutokana na Jeshi hilo lipo karibu na Jamii hivyo na jamii itafaidika na misaada hiyo kupitia Polisi.

Sauti ya Mwakilishi wa Jumuiya ya Korea Friend of Hope International Ushindi Philipo Maiko.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na Mashine ya Xrey, Kiti kwa ajili ya kung’olea meno, computer 20, na Vifaa mbalimbali kwa ajili ya karakana ya kutengenezea magari.