Zenj FM

Jamii yatakiwa kutumia vyombo vya sheria kudhibiti udhalilishaji Nungwi

20 August 2024, 3:07 pm

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Othman Ali Maulid Akizungumza na wananchi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Na Omar Hassan

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Othman Ali Maulid amewataka wananchi wa Nungwi kuacha tabia ya kusuluhisha kesi za udhalilishaji katika ngazi za familia na badala yake wazifikishe katika vyombo vya sheria ili zishughulikiwe kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na wananchi wa Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja katika utoaji wa elimu ya kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia na ukatili kwa watoto inayototewa na Jumuiya ya Maendeleo ya Jamii na Huduma Zanzibar JUMAJAHUZA kwa kushirikiana na Dawati la Jinsia na Watoto la Polisi, Mkuu huyo wa Wilaya amewasisitiza wananchi kutunza ushahidi ili kesi zifanikiwe Mahakamani.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini A, Othman Ali Maulid

Nae Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Sadik Ali Sultan amewaasa wananchi kuacha tabia ya kudhalilishana kupitia mitandao ya kijamii kwani amesema kumekuwa kukijitokeza makosa ya udhalilishaji kupitia mitandao.

Sauti ya Wakili na Mwanasheria wa Jeshi la Polisi Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Sadik Ali Sultan

Sharif Kombo Bakari na Tum Haji Juma wakaazi wa Nungwi wameviomba vyombo vya sheria kuzidisha bidii katika kukabiliana na matukio ya udhalilishaji ili kuyadhibiti Matukio hayo.

Sauti wananchi.

Jumuiya ya Maendeleo ya Jamii na Huduma Zanzibar JUMAJAHUZA imeamua kushirikiana na Polisi kutoa elimu ya kupinga udhalilishaji katika maeneo mbalimbali ambapo August 24 mwaka huu watatoa elimu kijiji cha Paje Mkoa wa Kusini Unguja.