Zenj FM

Katiku Mkuu Kiongozi: Shirikianeni na uwezeshaji kuwatafuta wanaohitaji kuwainua kiuchumi

16 August 2024, 6:26 pm

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said (aliyesimama) katika hafla ya kukabidhi viti na meza kwa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar. Picha na Omar Hassan.

Na Omar Hassan.

Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said ameitaka Ofisi ya Msajili wa asasi za Kiraia kushirikiana na Wakala uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kuwatambua wenye uhitaji na kuwasaidia wananchi.

Zena ametoa agizo hilo huko Chuo cha Polisi Zanzibar katika hafla ya kukabidhi viti na meza vyenye thamani ya Zaidi ya Milioni 67 kwa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar vilivyotolewa na Taasisi ya Muzdalifah Charitable Organization kwa kushirikiana na Taasisi ya Helping Hand for Relief and Development.

Sauti ya Katibu Mkuu kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said.

Nae Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad amesema Jeshi la Polisi linatambua na Kuthamini michango inayotolewa na Taasisi za kiraia na Serikali kwa Jeshi hilo na kwamba bado kuna uhitaji katika njanja ya elimu na Afya.

Sauti ya Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamad Khamis Hamad.
Viti na Meza vilivyotolewa kwa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar.

Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Taasisi ya Muzdalifah Farouk Hamad Khamis ameiomba Serikali kuendelea kupunguza ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini kwa lengo la kuwasaidia wananchi.

Sauti ya Mwakilishi kutoka Taasisi ya Muzdalifah Farouk Hamad Khamis.

Chuo cha Polisi Zanzibar mbali ya kutoa taaluma mbalimbali kwa Askari wa Jeshi hilo pia kinatoa mafunzo kwa taasisi nyengine pamoja na wananchi ikiwemo mafunzo ya udereva na Ulinzi.