Jamii yatakiwa kujitokeza kutoa ushahidi kesi za udhalilishaji
16 August 2024, 4:59 pm
Na Steven Msigaro
Jeshi la Polisi Mkoa Mjini Magharibi kupitia Dawati la Usalama Wetu Kwanza limesema linaendelea na mapambano dhidi ya udhalilishaji wa watoto kwa kutoa elimu maskulini.
Wakizungumza katika kipindi cha Mwangaza wa Babari kinachorushwa na Zenji fm Sajenti Mussa haji na Is-haka Mohammed wamesema mwitikio wa elimu juu ya la udhalilishaji kwa upande wa maskuli umepiga hatua kubwa kutokana na elimu inayotolewa kwa watoto imewasaidia kujilinda na matukio ya udhalilishaji.
Wamesema lisha ya muamko mkubwa wa uripotiwaji wa matukio ya udhalilishaji katika vituo vya Polisi nchini, kumekuwepo na changamoto ya kukosekana kwa Ushirikiano kati jeshi la polisi na familia hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa kwa kesi nyingi kuchukuliwa hatua za kisheria.
Aidha Jeshi la polisi kupitia dawati la Usalama Wetu Kwanza, limewataka wazazi na wananchi kushiriki kwenye mikutano ikiwemo maskuli kwa ajili ya kupata elimu na kuongeza uelewa wa kupambana na udhalilishaji dhidi ya watoto.