Zenj FM

Jeshi la polisi Zanzibar lakanusha taarifa za utekaji watoto

2 August 2024, 4:42 pm

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Zuberi Chembera

Na Omar Hassan

Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar limekanusha taarifa za kutekwa kwa watoto visiwani Zanzibar na linamshikilia Habibu Rashid Omar (35) mkazi wa Mwera ambaye anatuhumiwa kuchapisha taarifa ya uongo kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na kutekwa kwa watoto wanne huko Skuli ya Regezamwendo, hali iliyoleta taharuki kwa jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya polisi Zanzibar Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Zuberi Chembera amesema Zanzibar ni salama na hakuna tukio lolote la utekwaji wa watoto na kwamba amewataka wananchi kuzipuuza taarifa za upotoshaji zinazotolewa kupitia mitandao ya kijamii.

Sauti ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Zuberi Chembera.

Aidha DCP Chembera amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na linatarajia kuwafikisha mahakamani watuhumiwa watakaobainika kuhusika na tukio hilo.

Sauti ya Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Naibu Kamishna wa Polisi DCP. Zuberi Chembera.