Zenj FM

Wazazi watakiwa kuimarisha mahusiano na watoto

31 July 2024, 6:50 pm

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Vicent Innocent akiwa studio za Zenji Fm.

Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Vicent Innocent amewasihi  wazazi kuwa walimu wazuri juu ya malezi ya watoto ili kuwalinda na kuwakuza watoto kwenye ustawi wa maadili mema.

Akizungumza  kwenye mahojiano na kituo cha Radio Zenji FM amesema usimamizi  mbovu wa wazazi umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa  vitendo vya udhalilishaji na ukatili katika jamii.

Sauti ya Mtangazaji Ivan Mapunda akifanya mahojiano na Inspekta Vicent Innocent.

Inspekta Vicent Innocent amesema sheria na haki za kibinadamu juu ya watoto hazimuondolei mzazi stahiki zake za msingi katika malezi ya mtoto bali zipo katika kumlinda mtoto kwa ustawi bora wa makuzi kwa kuzingatia stahiki zake. Aidha Mkaguzi Msaidi wa Polisi Vicent Innocent anawahasa wazazi juu ya kutokata tamaa katika malezi ya watoto na kuhakikisha  kuwa na ukaribu mzuri kati ya mzazi au mlezi na mtoto kutokana na vitendo vingi vya udhalilishaji na ukatili dhidi ya watoto vinafanywa na watu wa karibu kwenye jamii.

Sauti ya Mtangazaji Ivan Mapunda akifanya mahojiano na Inspekta Vicent Innocent.