Zenj FM

Jeshi la Polisi Zanzibar lapania kupunguza ajali

12 June 2024, 5:32 pm

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi

Na Omary Hassan

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi amesema Jeshi la Polisi linashirikiana na Taasisi nyengine zinazosimamia usalama barabarani kuweka mikakati ya kupunguza ajali za Barabarani ambazo zimekuwa zikileta madhara kwa jamii na Serikali.

Akizungumza akiwa katika ziara ya kikazi visiwani Zanzibar amesema wamekubaliana na Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani Zanzibar kufanya Operesheni kwa madereva wa vyombo vya moto ili kuwadhibiti wanaokiuka sheria na taratibu za Usalama Barabarani.

Sauti ya Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi.

Nae Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Arusha Technical Collage Mussa Chacha amesema Chuo hicho kilatoa fursa za Masomo kwa watu wa Zanzibar hasa walimu wa vyuo vya udereva ili wawe na taaluma ya usalama barabarani na hatimae kupunguza ajali za barabarani.

Sauti ya Mkuu wa Chuo cha Ufundi cha Arusha Technical Collage Mussa Chacha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri na Usalama barabarani Zanzibar Haji Ali Zubeir amesema Mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi na Chuo cha Ufundi Arusha ili kudhibiti ajali za barabarani hasa ajali zinazosababishwa na waendesha bodaboda.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri na Usalama barabarani Zanzibar Haji Ali Zubeir.