Zenj FM

Jeshi la Polisi Zanzibar lajipanga fainali ya Yanga SC vs Azam FC

31 May 2024, 2:40 pm

Kamanda wa Polisi,Mkoa wa Mjini Magharibi,SACP Richard Thadei Mchomvu.

Na Mary Julius

Fainali ya kombe la FA Tanzania Bara (CRDB Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa tarehe 02.06.2024 katika uwanja wa New Amaan Complex saa 2:15 usiku kati ya YANGA SC vs AZAM FC.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limesema limejipanga vizuri kuhakikisha wananchi, wanachama, mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu wanashiriki katika mchezo huo kwa usalama na amani.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Madema Kamanda wa Polisi,Mkoa wa Mjini Magharibi,SACP Richard Thadei Mchomvu amesema Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama litahakikisha linazuia matukio ya kihalifu ya aina yeyote yanayoweza kujitokeza kabla, wakati na baada ya mchezo huo kumalizika.

Aidha kamanda ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kutotumia nafasi ya mechi hiyo kuwa sehemu ya kuvunja na kutotii sheria za usalama barabarani, Kwani hatua kali za kisheria zitachukulia kwa yeyote atakaebainika kufanya hivyo.

Sauti ya Kamanda wa Polisi,Mkoa wa Mjini Magharibi,SACP Richard Thadei Mchomvu.