Wazanzibar watakiwa kujiandikisha katika daftari la wapiga kura
8 November 2023, 3:17 pm
Na Mary Julius.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji George Joseph Kazi amewataka wananchi walio timiza sifa za kupiga kura kujitokeza katika zoezi la uandikishaji kwenye daftari la kudumu la mpiga kura ili waweze kushiriki katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025.
Mwenyekiti ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi kuhusu uandikishaji wa wapiga kura wapya katika daftari la kudumu, uliofanyika katika ukumbi wa Idrisa Abdulwakili Kikwajuni Zanzibar amesema zoezi hilo linalotarajiwa kuanza mwenzi wa 12 tarehe 2 na kumalizika tarehe 15 mwezi wa kwanza 2024 ikiwa ni sehemu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025
Aidha jaji amesema uandikishwaji wa wapiga kura itahusisha wapiga kura wapya ambao hawajawahi kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Akijibu hoja zilizotolewa na washiriki wa mkutano huo Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Thabit Faina amesema tume hiyo inatarajia kuandikisha wapiga kura wapatao laki moja sitini na mbili elfu mia sita na sita kutokana na maladilio ya takwimu ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.
Wakichangia mada zilizo wakilishwa baadhi ya wanasiasa wameiomba tume kuongeza bidii katika utoaji wa elimu ya kujiandikisha katika zoezi hilo.
Aidha wamewataka masheha kuzielewa sheria pamoja na vyama kupatiwa ruzuku ili viweze kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.