Airpay Tanzania kuwa mkombozi wa uchakavu wa noti nchini
25 October 2023, 5:26 pm
Na Mary Julius.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dkt. Saada Mkuya Salum amesema kuzinduliwa kwa mfumo wa kufanya malipo kwa njia ya mtandao wa Airpay Tanzania utaisadia noti za Tanzania kuwa katika mzunguko kwa muda mrefu.
Waziri Saada ameyasema hayo wakati akimwakilisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi katika uzinduzi wa Airpay Tanzania uliofanyika hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege.
Amesema Airpay itaweza kusaidia kupunguza matumizi ya malipo taslimu sokoni na badala yake kutumia mtandao ambapo utasaidia kuiwezesha fedha kutokuchakaa na kuingiza serikali hasara ya kuzalisha fedha mpya kila mara.
Aidha amesema mfumo huo utawasaidia wajasiriamali wadogo wadogo kutumia mfumo wa kidigital wa kufanya malipo pamoja na kuongeza usalama wa fedha.
Kwa upande wake mwanzilishi wa Airpay Tanzania Yasmin Chali amesema mfumo huu utaweza kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo visiwani Zanzibar katika kufanya malipo kwa njia ya matandao
Aidha amesema Airpay Tanzania inatarajia kuanzisha chuo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wajasiliamali ili waweze kutumia mifumo ya fedha ya kidigital.
Kwa upande wake Waziri Nchi Ofisi ya Raisi Kazi Uchumi na Uwezeshaji Mudrik Ramadhan Soraga amesema mfumo huu utasaidia serikali ya mapinduzi ya zanzibar kuwa na takwimu sahihi za wajasiriamali walio sajiliwa pamoja na kujua idadi ya wajasiriamali ambao wanalipa kodi.