Pemba waomba kuongezewa ATM
2 October 2023, 3:48 pm
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, wateja wa benki ya NMB wametakiwa kutoa maoni yao kila wanapoona changamoto katika utoaji wa huduma kwa kupitia visanduku hivyo vya maoni .
Na Is- haka Mohammed
Afisa Mdhamin Ofisi ya Rais Ikulu Shuwekha Abdalla Omar ameutaka uongozi na wafanyakazi wa Benk ya NMB Tawi la Chake Chake kuwa wepesi wa kuyafanyia kazi malalamiko yanatolewa na wateja na kuyapatia ufumbuzi kwa muda sahihi ili benki hiyo iweze kuimarika zaidi aktika utoaji wa huduma.
Mdhamini huyo ametoa wito huko Chake Chake wakati akizungumza na wafanyakazi na wateja wa benki ya NMB Tawi la Chake chake katika uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya huduma kwa wateja duniani na kusema kuwa maoni hayo ni muhimu kwa maendeleo ya benki hiyo.
Naye Maneja wa NMB Tawi la Chake Chake Hamad Mussa Msafiri amesema benki hiyo imekuwa ikitambua juu ya umuhimu wa utoaji wa huduma bora kwa wateja na ndiyo wafanyakazi wa benki hiyo wamekuwa wakiwathamini wateja wao.
Mapema Meneja wa Huduma kwa Wateja katika Benki ya NMB Tawi la Chake Chake Wahbi Ahmad Alaw amesema mafanikio yaliyopatikana yametokana na utoaji wake wa huduma na mahusiano mazuri na wateja wake.
Nao baadhi ya wateja wa NMB walioshiriki kwenye uzinduzi huo wameshauri kuongezwa kwa vituo vya kutolea pesa kwenye maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba huku wakiomba maeneo zaidi yatumike wakati uwekaji au utoaji wa pesa pale idadi ya wateja wanapokuwa wingi benki.