Airpay Tanzania yaleta neema kwa wajasriamali Zanzibar
21 September 2023, 2:25 pm
Na Mary Julius.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Mudrik Ramadhani Soraga amesema ujio wa kampuni ya Airpay Tanzania, Zanzibar itasaidia serikali kuwafikia wajasiriamali wadogo katika kupata fursa za mikopo na kutambulika.
Soraga ameyasema hayo wakati akifungua ofisi ya kampuni ya Airpay Tanzania katika jengo la Muzamir Mlandege Zanzibar, amesema AIRPAY itawezesha wajasiriamali kujisajil na kuweza kutambulika kupata huduma za fedha kidigital.
Aidha amesema kampuni hiyo ambayo ni ya kwanza kuwa na makao makuu Zanzibar itasaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ukusanyaji wa Kodi .
Akizungumza katika uziinduzi huo Makamu Rais na Meneja Mikakati Wa Kampuni ya Airpay Tanzania Mihayo Wilmore amesema lengo la kampuni hiyo ni kuhakikisha inawafikia wajasiriamli wadogo na kuwaingiza katika mfumo wa air pay ambao utawezesha wafanyabiashara wa aina zote kutumia
Aidha amesema mfumo wa AIRPAY utasaidia wajasiriamali kuweza kukopeshwa na mabenki kwani taarifa zao za siku mwezi mpaka mwaka zitaonekana katika mfumo huo Hali amabayo itamsaidia mjasriamali kutunza kumbukumbu zao za biashara.
Kwa upande wake Meneja Uchumi wa Banki Kuu ya Tanzania Ofisi ya Zanzibar Moto Ngwinganele Lugobi amesema bot imejiridhisha kuwa AIRPAY inauwezo wa kufanya huduma za kifedha na ndio maana wamewapatia leseni ya kufanya hivyo .
Kampuni ya Airpay ina uzoefu wa muda wa miaka 12 na makao yake makuu ni nchini India