Wilaya ya Kusini Unguja yaomba nyumba za walimu
10 September 2023, 2:19 pm
Na Mary Julius.
Afisa Elimu Mkoa wa Kusini Unguja Mohammed Haji Ramadhani ameiomba wizara ya elimu kuwajengea nyumba walimu wa mkoa huo ili waweze kufika kwa wakati maskulini.
Afisa elimu ameyasema hayo katika hafla ya kugawa taulo za kike zilizoteolewa na Asma Mwinyi Foundation katika ukumbi wa mitihani wa Skuli ya Kizimkazi Dimani.
Amesema umbali wa makazi ya walimu unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ufaulu kwa wanafunzi wa mkoa huo kutokana na kuchelewa kuingia darasani kwa wakati .
Akizungumzia msaada huo wa taulo za kike amesema utawasaidia watoto wa kike kujiamnini na kuongeza bidii katika masomo yao hasa wale ambao wapo katika makambi kwa ajili ya kujiandaa na mitihani ya taifa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation Asma Ali Mwinyi amesema wameamua kutoa taulo hizo ili kuwawezesha wanafunzi wengi wa kike kuhudhuria masomo na kuongeza ufaulu wa masomo yao ili kutokomeza ziro katika maskuli ya Zanzibar.
Nao wanafunzi waliopatiwa taulo hizo wamemuahidi mkurugenzi wa Asma Mwinyi kuwa watasoma kwa bidii kwani kwa kupatiwa taulo hizo wataweza kuhudhulia vipindi yote vya masomo.
Skuli zilizopatiwa taulo hizo kwa wilaya ya kusini unguja ni Skuli ya Muyuni Sekondary, Hasnuu Makame,Kizimkazi Dimbani,Kizimkazi Mikunguni na Kusini ambapo zaidi ya wanafunzi 380 wamepatiwa pakiti 3 kila mmoja.