Wanafunzi wa kiume wilaya ya Kati Unguja wapewa mbinu kufikia ndoto zao
10 September 2023, 1:47 pm
Na. Hakika Mwinyi
Afisa Elimu wa Wilaya ya Kati Somoe Said amewataka wanafunzi wa kiume kujiepusha na vishawishi ili kuweza kutimiza malengo waliyojiwekea.
Afisa Elimu ameyasema hayo katika ghafla ya kuwatunuku vyeti wanafunzi Wakiume 20 walio shiriki katika marathon iliyo andaliwa na Taasisi ya Happy Teenagers Talk, hafla iliyofanyika katika uwanja wa ofisi za Wilaya Dunga Wilaya ya Kati Unguja, Amesema maisha ya yanachangamoto nyingi ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya vitendo vya udhalilishaji, mimba za utotoni.
Aidha Amesema taasisi nyingi zimekuwa zikijikita katika kuwaelimisha watoto wa kike na kuwasahau watoto wa kiume hivyo ameipongeza taasisi ya happy tennega kwa kuwaaamua kuwaelimisha watoto wa kiume ili waweze kujitambua na kuachana na vitendo viovu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Happy TeenagersTalk Happiness Johnson Mwita amesema lengo la kuanda Marathoni kwa wanafunzi hao ni kuwaweka karibu na kuzungumza nao ili kuhakikisha vijana wanaepukana na vishawishi ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya, ndoa za mapema na ngono zembe katika umri mdogo.
Nae Mwalimu wa Michezo kutoka Skuli ya sekondari Uzini Ali Mabrouk Mshimba kwaniaba ya Walimu wenzake amewataka wazazi kuwahamasisha watoto kushiriki katika michezo.
Kwa uapande wake mwanafunzi Bilali Abdallah Hassan kutoka Skuli ya Uzini ambae aliibuka mshindi wa kwanza katika mashindano hayo kwaniaba ya wenzake amewaomba wanafunzi wenzake kutovunjika moyo, wazidishe jitihada katika masomo.
Jumla ya zawadi za aina nne zimetolewa kwa washindi hao ikiwemo medali za dhahabu na Fedha, sturdy tour kwa washiriki ndani na nje ya Zanzibar, fedha taslim pamoja na vyeti kwa washiriki wote 159 wa skuli 15 za Wilaya ya Kati.