Asma Mwinyi arejesha matumaini kwa wanafunzi wa kike Zanzibar
7 September 2023, 5:07 pm
Na Mary Julius
Mkurugenzi wa Asma Mwinyi Foundation, Asma Ali Mwinyi amesema taasisi hiyo inaandaa mkakati wa kuweka mazingira rafiki kwa watoto wa kike kwa kuwajengea vyoo maskulini ili kuondoa changamoto zote zinazowakumba wanapo kuwa katika hedhi.
Asma ameyasema hayo mara baada ya kugawa taulo za kike kwa wanafunzi wa skulii ya sekondari ya kwarara ikiwa ni muendelezo wa kugawa taulo hizo kwa wanafunzi wa skuli za jimbo la dimani akishirikiana na umoja wa wanawake wa jimbo hilo amesema lengo ni kuweka mazingira rafiki yatakayo wezesha mwanafunzi kike kusoma vizuri.
Aidha Asma amewaahidi wanafunzi wa skuli ya sekondar ya kwarara wanaotarajia kufanya mitihani ya kidato cha nn iwapo watafauli kwa daraja la mwanza atawapatia mabunda matano ya taulo za kike kwa kila mmoja.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Skuli ya sekondari ya kwarara Khadija Sharif Omary ,ameipongeza taassisi hiyo kwa kuweza kutoa taulo hizo na amewaomba zoezi hilo liwe la mara kwa mara kwani uhitaji ni mkubwa.
Kwa upande wake diwani wa viti maalum Veronika Pang`las Mtindira amesema UWT dimani kwa kushirikiana na asma mwinyi faoundation imejipanga kutoa taulo za kike kwa skuli zote zilizopo katika wilaya ya dimani kichama lengo likiwa ni kuwawezesha watoto wa kike kusoma kwa bidii na kuongeza ufaulu katika masomo yao.
Nao wanafunzi wa skulii ya kwarara wameishukuru asma mwinyi faundatuon kwa kuweza kuwapata taulo hizo zitakazo wasaidia kujistili.
Zaidi ya wanafunzi 600 wa skuli ya kwarara secondary wamepatiwa taulo hizo za kike.