Tamwa Zanzibar yawanoa waandishi wa habari Pemba
25 August 2023, 3:56 pm
Waandishi wa Habari Pemba wanatakiwa kufanya uchunguzi yakinifu kabla ya kurusha hewani habari za udhalilishaji.
Na Is-haka Mohammed Pemba.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa Zanzibar) kimewakumbusha waandishi wa habari juu ya umuhimu wa kuandika habari zenye tija na kupelekea mabadiliko ya kweli kwenye masuala ya kukabiliana na matendo ya udhalilishaji wa kijinsia.
Afisa Mkuu wa Mawasiliano na Utetezi Tamwa Zanzibar Saphia Ngalapi ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mafunzo ya siku tatu yaliyolenga kuwapiga msasa waandishi habari 16 wa kisiwani Pemba juu ya kuandika kwa uweledi habari zinazohusu udhalilishaji yanayoendelea katika ofisi za Tamwa Mkanjuni Chake Chake.
Amesema mafunzo hayo yanalenga kuongeza uelewa kwa waandishii wa habari kuandika habari habari bora kwa kufuata maadili za udhalilishaji ambazo zitasaidia katika kuleta mabadiko chanya kwa jamii na taasisi mbali mbali.
Naye Mwenyezeshaji katika mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Taifa (SUZA) Aimani Duwe amesema sifa moja ya mwandishi wa habari ni kuwa mbunifu na kuwataka kuwa wabunifu wanapoandika habari zinazohusu uhdalilishaji wa kijinsia.