Sabra Machano arudishwa kazini
15 August 2023, 4:58 pm
Na Ivan Mapunda.
Aliyekuwa Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Sabra Issa Machano amefutiwa mashtaka ya ubadhilifu wa fedha wa bilioni 3 .
Akizungumza na Zenj fm mkurugenzi wa taasisi ya Warrior Women Sabra Issa Machano amesema amepokea barua kutoka Ofisi ya Rais na kumjulisha kuwa uchunguzi umeisha na anatakiwa kurudi kazini.
Sabra amesema sakata lilokuwa likimkabili la ubadhirifu wa fedha wa bilioni tatu wa mradi mkubwa wa serikali wa mjini ambao changamoto kubwa ilikua ni mkataba ambao ulifungwa mwaka 2015 wakati yeye kaingia zssf mwishoni mwa mwaka 2017
Aidha amemshukuru Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Hussein Mwinyi kwa kumaliza suala hili zito dhidi yake.
Ikumbukwe kuwa Dec 23 mwaka 2020 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alimsimamisha kazi Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Sabra Issa Machano na watendaji wengine kwa tuhuma za kuhusika na makosa mbali mbali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya Serikali.