Bandari Pemba yakusanya zaidi ya bilion 2
14 August 2023, 1:54 pm
Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar imetembelea bandari ya Mkoani Pemba na kushuhudia madadiliko katika bandari hiyo ikiwemo katika njia ya kupitia abiria ambapo sasa abiria wanaweza kupita bila ya kupigwa na jua au mvua inaponyesha.
Na Is-haka Mohammed Pemba
Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi imepongeza Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi kwa juhudi inazozichukua katika kuimarisha huduma za usafiri Nchini.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mwanaisha Khamis Juma mara ametoa pongezi hizo mara baada ya kupokea ripoti ya wizara hiyo huko Mkoani .
Amesema Wizara ya Ujenzi imekuwa ikifanya maborosho katika kuhakikisha huduma za usafiri wa bahari na nchi kavu kuona zinaimarika.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dr Khalid Salum Mohd amesema katika kipindi cha mwaka 2022/23 Wizara hiyo imekadiria kukusanya jumla ya shilingi bilioni mbili milioni miasaba na sabiini na saba katika bandari ya Pemba, kupitia Vyanzo mbali mbali Vya mapato kwenya bandari hiyo.
Aidha Dr Khalid amesema Wizara imejipanga kufanya ukarabati wa miundombinu katika maeno ya bandari ili kuona huduma hiyo inakuwa yenye ubora.