Zenj FM

Tadio yawapiga msasa waandishi wa habari Zanzibar

9 August 2023, 2:49 pm

Mhariri wa Radio Tadio Hilali Ruhundwa (aliye simama) akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari Zanzibar. Picha na Fatuma Ali

Waandishi wa habari Zanzibar wametakiwa kutumia mtandao wa Radio Tadio ili kubadilishana habari.

Na Mary Julius

Mhariri wa Radio Tadio Tanzania Hilali Ruhundwa amewataka waandishi wa habari zanzibar kuitumia fursa ya mtandao wa radio tadio  katika kuchapisha habari ili kuweza kuifikia  jamii.

Akizungumza  mara baada ya kufunga mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwelewa waaandishi wa habari juu ya kuchapisha habari online kwa waandishi wa habari wananchama wa radio tadio iliyofanyika kariakoo Zanzibar.

Amesema lengo la kuanzishwa kwa radio tadio ni kuziunganisha radio za kijamii za Tanzania ili kuitumia katika kubadiilishana habari.

Sauti ya Mhariri wa Radio TADIO Tanzania Hilali Ruhundwa.

Kwa upande wake afisa msimamizi wa Tadio Fatuma Ali  amewataka waandishi wa habari kuyafanyia kazi mafunzo hayo ili lengo la kuhabarisha jamii  liweze kufikiwa.

Sauti ya Afisa msimamizi wa TADIO Fatuma Ali

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Katibu Mtendaji wa TADIO Ali Khamis amesema watahakikisha wanayafanyia kazi mafunzo waliopatiwa, pamoja na kurusha hewani matangazo ya vituo vyao.