Jinsi Samia alivyoshusha gari jipya Tafiri Kyela
5 October 2024, 10:20
Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasani ametoa gari jipya kwa Kituo cha Utafiti wa Samaki wilaya ya Kyela Tafiri ili kurahisisha utendaji kazi wa kituo hicho.
Na Nsangatii Mwakipesile
Kaimu mkurugenzi kituo cha utafiti wa uvuvi Tafiri Kyela Dkt. Nestory Gabagambi amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia gari jipya kwajili ya kurahisisha uendeshaji wa shughuri mbalimbali wa taaasisi hiyo.
Akizungumza na keifo fm radio Dkt. Gabagambi amesema tangu kuanza kwa kituoa hicho cha utafiti hapa wilayani kyela hawajawahi kuwa na gari hali iliyokuwa inapelekea ugumu wa utekelezaji wa majukumu kwa wakati hivyo kupatikana kwa chombo hicho hivi sasa kutarahisisha utendaji kazi wa Tafiri.
Dr Gabagambi ameleza majukumu makubwa ya TAFIRI kwa wilaya ya kyela ni kufanya tafiti za uvuvi kwenye kanda ya nyanda za juu kusini na kusini magaribi mikoa saba.
Wakati huohuo Dr Gabagambi amewaomba watanzania hususani wanakyela kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa mwaka wa utafiti unaotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa AICC.
Taasisi ya utafiti wa uvuvi Tanzania alianzishwa mwaka 80 kwa sheria ya bunge na 6 na ikaendelea kufanya kazi mpaka mwaka 2016 kabla ya kufanyiwa marekebisho na kuongezewa majukumu ambayo mpaka sasa inafanya kazi katika sheria hiyo.