Kyela:Kinanasi aungana na waislamu funga ya mwezi mtukufu
20 March 2024, 13:09
Wakati waumini wa dini ya kiislamu wliayani kyela wakiendelea na mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Kinanasi ametoa sukari na mitungi ya gesi kwa kila msikiti wilayani kyela.
Na Masoud Maulid
Mbunge wa jimbo la Kyela Ally Mlaghila Kinanasi ameungana na waislamu wilaya ya kyela wanaotekeleza nguzo ya nne katika dini ya KIislamu ya kufunga mwezi mtukufu wa ramadhani kwa kutoa sadaka ya sukari na mtungi wa gesi kwa kila msikiti.
Akizungumza na mwandishi wa habari katibu wa mbunge Edger Mwasamlagila amesema zoezi la kugawa sadaka hiyo angeifanya mbunge mwenyewe kupita kila msikiti wilaya ya kyela lakini kutokana na majukumu ya kushiriki vikao vya kamati jijini Dodoma,hivyo zoezi hilo linatekelezwa na katibu wake ambapo ugawaji wa sukari kilo 40 pamoja na mtungi mmoja wa gesi vimetolewa msikiti mkubwa wa wilaya.
Mwasamlagila ameongeza kuwa zoezi la kutoa sadaka hiyo linaendelea kufanyika katika misikiti ambayo wameweka utaratibu wa kuwafuturisha waislam eneo moja la msikiti tangu kuanza kwa ramadhani,ambapo watakabidhiwa sukari pamoja na mtungi wa gesi lengo likiwa pia ni kuunga jitihada za rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania katika kutumia nishati mbadala ambapo rais ni mjumbe wa kamati.
Kwa upande wake imamu wa msikiti mkuu wa wilaya kupitia baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA Omary Ngelangela,ametoa shukrani kwa niaba ya waislamu kwa sadaka ambayo imetolewa na mbunge wa jimbo la Kyela na kuahidi kuendelea kumpatia ushirikiano na kumuombea kwa mwenyezi mungu ampe afya na nguvu zaidi ya kuwatumikia wananchi wa jimbo lake.
Nae ustadhi Ayubu haruna mjumbe wa kamati ya msikiti wa Aqswa uliopo kitongoji cha mikumi kata ya bondeni amesema hawakutarajia kupa msaada huo ndani ya mwezi huu wa ramadhani hivyo wamempongeza mbunge kwa maono yake hivyo nao pia wanamuombea kwa mwenyezimungu awe na moyo wa kuendelea kuwakumbuka waislmau na katika mambo mengine
Misikiti inayotaraji kupokea sadaka hiyo ya sukari kilo 40 pamoja na mtungi wa gesi ni pamoja msikiti mkuu wa wilaya,masjidi aqswa,masjidi madinatul-mnawara boda,masjidi raub`wa njisi,msikiti wa stamiko,msikiti wa makwale,msikiti wa itope,ipinda na msikiti wa tenende.