Kyela:Ccm Itunge yang’ara kwa manoti ya Mwakyambile
20 March 2024, 11:52
Mkurugrnzi wa kampuni ya Convenant Edible Oil Ltd wazalishaji wa mafuta ya Kyela Cooking Oil Babylon Mwakyambile amewataka wanachama wa chama cha mapinduzi kata ya itunge kushikama ili kufanikisha ujenzi wa ofisi za chama hicho.
Na Nsangatii Mwakipesile
Harambee ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya chama cha mapinduzi kata ya Itunge wilayani kyela imefanyika huku mdau wa maendeleo na mkuregenzi wa kampuni ya Convenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya Kyela Cooking Oil Babylon Mwakyambile akitoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja.
Huu ni umekuwa mwendelezo wa mdau na mkurugenzi huyo wa kiwanda cha kuzarisha mafuta cha Kyela Cooking Oil kuendendelea kushiriki na kuchangia katika shughuli mbalimbali za kijamii hapa wilayani kyela.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo vya ujenzi Mwakyambile amewapongeza wanachama wa chama cha Mapinduzi kata ya Itunge kwa wazo hilo la kuanzisha ujenzi huo ambao amesema utakuwa ni alama kwa vizazi vijavyo na kuwataka vijana wengine wa Itunge kuchangia chama chao.
Kuhusu vifaa vya ujenzi alivyovitoa amemtaka fundi wa jengo hilo kuanza ujenzi huo mara moja huku akibainisha kuwa tofari,mchanga,nondo,saruji na kokoto vipo ambapo katika kuhakikisha hilo linaanza mara moja Mwakyambile amekabidhi fedha taslimu shilingi laki mbili kwa ajiri ya malipo ya awali kwa fundi.
Kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Itunge Gwandumi Mwasemele amemshukuru Babylon Mwakyambile kwa mchango wake huo akisema harambee hiyo imefanikiwa kwa asilimia mia kwani watu wamejitoa katika kufanikisha hilo.
Hii si mara ya kwanza kwa mdau huyo wa maendeleo na mkurugenzi wa kampuni ya Convenant Edible Oil Ltd wazarishaji wa mafuta ya Kyela Cooking Oil kushiriki katika kuchangia shughuli mbalimbali za kijamii hapa wilayani kyela kwani mpaka sasa amekwisha fanya hivyo katika kata za Isaki,Ngusa na ofisi za chama wilaya ya kyela ambapo ameahidi kuendelea kushikamana nao katika kila hali.