Mwaisango: Iwe mvua, jua tunaingia kwenye uchaguzi
13 March 2024, 14:19
Chama cha CHADEMA wilayani kyela kimeitaka serikali ya chama cha mapinduzi wilayani hapa kujiandaa kikamilifu katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na ule mkuu wa mwaka 2025 kuwa ni lazima wakiondoshe madarakani.
Na James Mwakyembe
Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA wilayani kyela kimesema kitaingia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadae mwezi octoba mwaka huu.
Haya yanajiri ikiwa ni siku chache baada ya kukamilika kwa zoezi la uchaguzi wa ndani wa chama hicho wilayani hapa ambapo chama hicho kimekuwa hakishiriki katika chaguzi mbalimbali zilizopita wakishinikiza serikali na jumuiya za kimataifa kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi hapa nchini Tanzania.
Akizungumza katika ofisi za chama hicho zilizopo katika kata ya kyela mjini katibu mwenezi wa chama hicho Donald Elukaga Mwaisango amesema kwa muujibu ya kauli iliyotolewa na viongozi wa chama hicho taifa kuwa iwe mvua au jua lazima chama chao kingie katika chaguzi zote zilizombele yao ili kuhakikisha wanarejeza hali ya democrasi hapa nchini
Akijibu swali la mwandishi habari wa keifo fm lililouliza je?wanazani kuwa madai yao yameshughulikiwa ipasavyo na serikali hata kuwashawishi wao kuuingia kwenye uchaguzi ujao,Mwaisango amesema wanaridhishwa na hatua za awali ambazo zimeendelea kuchukuliwa na serikali chini ya raisi Samia Suluhu Hasani kuwa zinaonesha dira ya kuwepo uchaguzi huru na haki.
Kuhusu hali ya democrasia nchini Mwaisango amesema zipo hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali kama vile kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa pamoja na maandamano ya amani jambo ambalo linaonesha kuimarika kwa demokrasi nchini.
Donald Mwaisango ni katibu mwenezi wa chama cha CHADEMA aliyefanikiwa kutetea nafasi yake kwa mhura wa tatu mfurulizo ameungana na mwenyekiti mpya mwanamke wa kwanza katika chama hicho victoria Swebe na kuhitimisha mchakato wa kuwapata viongozi wa chama hicho wilaya ya Kyela.