Swebe: Wanawake jitokezeni kugombea serikali za mitaa
11 March 2024, 17:30
Mwenyekiti mpya CHADEMA wilaya ya Kyela Victoria Swebe amewataka wanawake wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uenyekiti wa serikali za mitaa katika uchaguzi ujao.
Na James Mwakyembe
Baada ya kuchaguliwa na kuwa mwenyekiti mpya mwanamke wa chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA mwenyekiti mpya wa chama hicho Victoria Swebe amewashukuru wanachama wote wa chama hicho wilayani kyela.
Swebe amechaguliwa katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho na kuwa mwenyekiti wa chama cha CHADEMA kwa wilaya ya Kyela akiweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza ndani ya chama hicho hapa wilayani kuaminiwa na kuepewa dhamana hiyo kubwa kuwaongoza wanachaadema.
Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe mbele ya vyombo vya habari Victoria Swebe amewashukuru wanachama wote wa CHADEMA wilayani kyela kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuwaongoza huku akisema atahakikisha anasimamia kukijenga chama hicho kikubwa cha upinzani hapa nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa dira yake baada ya kuchaguliwa ni kufanya kazi kwa kujituma na wananchama wote huku akisema atahakikisha anavunja makundi yote yaliyokuwa yaliyokuwepo wakati wa uchaguzi na pamoja na kutengeneza miundombinu ya chama hicho ikiwemo ujenzi wa ofisi za chama wilaya.
Kuhusu rai yake kwa wanawake wanaowaongoza amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za kiserikali ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2024 akitaja sababu kuwa wanawake ni watu wanaweza bila kuwezeshwa.
Victoria Benson Swebe anakuwa mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kukiongoza chama cha CHADEMA wilaya ya Kyela baada ya kuwabwaga wagombea wengine walijitokeza kugombea nafasi hiyo akiwemo aliyekuwa akitetea nafasi yake Mbegese.