Mwakitalu: Tusherehekee sabasaba, tusiuze chakula
5 July 2024, 21:25
Mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa kutoka mkoa wa Mbeya Ramadhani Lufingo Mwakitalu amewaomba wanakyela kutouza chakula kwa fujo kuelekea siku ya sabasaba.
Na James Mwakyembe
Ikiwa zimesaria siku mbili kuelekea kilele cha siku ya sabasaba inayotarajiwa kufanyika jumapili ya July 7 Mwaka huu wananchi wilayani kyela wametakiwa kuchukua tahadhari ya matumizi ya chakula walichokivuna ili kujikinga na njaa.
Tahadhari hiyo imetolewa na mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa Ramadhani Lufingo Mwakitalu wakati akizungumza na kituo hiki nyumbani kwake Ipinda ambapo amesema licha ya kuwa siku hii ni muhimu kwa jamii ya wanakyela kusherehekea mwaka wa mavuno katika siku hiyo lakini ni vyema jamii ikachukua tahadhari ya matumizi mbaya ya chakula ili kuepukana na njaa.
Pamoja na kuitaka jamii ya wanakyela kuchukua hadhari pia Mwakitalu amepongeza chama cha Mapinduzi CCM chini ya Mwenyekiti wake Elias Ulisaja Mwanjala kwa namna ambavyo wamekuwa wakimpa ushirikiano katika nafasi yake ya mjumbe wa mkutano mkuu taifa kutekeleza majukumu yake.
Ametumia nafasi hiyo pia kuwakumbusha wanachama wote wa chama cha mapinduzi kuhakikisha wanajiandaa vema katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwezi octoba mwaka huu ili kuhakikisha chama hicho kinashinda kwa kishindo.
Kupata undani wa habari hii tunaungana na mwandishi wetu James Mwakaligemo ambaye amefanya mazungumzo na Ramadhan Mwakitalu kuhusu mambo mbalimbali kuelekea sikukuu ya Sabasaba
Kwanza amemuuliza kuhusu sabasaba ni nini?