Keifo FM

Kyela:Miti 150,0000,kupandwa Kyela

3 June 2024, 16:14

Pichani ni picha kutoka chumba cha habari ikionesha mpango wa kabambe wa serikali ya halmashauri ya Kyela ikijiandaa kujidhatiti na mafuriko kwa kupanda miti picha James Mwakyembe

Katika kukabiliana na janga la mafuriko ambalo limekuwa likiisumbua wilaya ya Kyela mara kwa mara serikali imekusudia kupanda miti milioni moja na laki tano.

Na James Mwakyembe

Siku chache baada ya mvua kubwa kuikumba wilaya ya Kyela serikali imekusudia kupanda miti zaidi ya milioni moja katika maeneo mbalimbali hapa wilayani.

Zoezi hili linakuja kufuatia uharibifu mkubwa uliojitokeza baada ya janga la mafuriko lililoikumba wilaya ya Kyela hali iliyopelekea wananchi kukosa chakula baadhi yao kuyahama makazi yao.

Ambapo katika kukabiliana na hali hiyo serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali walijitokeza katika kuhakikisha wanaungana na wanajamii wengine katika kutoa misaada ya hali na mali kwa waathirika wa mafuriko.

Kutokana na hali hiyo serikali ya halmashauri ya wilaya ya Kyela imeamua kuja na mkakati kabambe wa kuhamasisha wananchi kupanda miti katika maeneo mbalimbali ikiwamo katika vyanzo vya mito lengo likiwa ni kukabiliana na hali hatarishi wa mafuriko.

Naaa ,mwenzangu James Mwakyembe muada mfupi uliopita amezungumza kwa simu na afisa wa mazingira wilaya ya Kyela Godwin Gozbert kuhusu ni hatua gani serikali imechukua kukabiliana na hali ya majanga ya mafuriko hapa wilayani kyela

Kwanza amemuuliza je? ni hatua gani serikali kupitia kitengo cha mazingira imezichukua ili kujikinga na janga la mafuriko?    Interview James vs Gozbert

sikiliza interview hiyo ya afisa wa mazingira hapa wilayani kyela akizungumzia namna ambavyo Serikali inajipanga kukabiliana mafuriko hapa wilayani kyela.