Keifo FM

Kyela: Wafanyabiashara acheni kugoma njooni TCCIA

27 May 2024, 18:21

Pichani ni mwenyekiti wa TCCIA CPA Don Koroso akiwa katika ofisi zake hapa wilayani kyela picha na Masoud Maulid

Mwenyekiti wa taasisi ya biashara,viwanda na kilimo Tanzania TCCIA amewataka wafanyabiashara wilayani kyela kuitumia taasi yao ili kuondokana na migogoro ya kibiashara isiyo ya lazma.

Na Masoud Maulid

Siku mbili baada ya mgomo wa wafanyabiashara wa soko la kyela kugoma kufungua biashara zao kutamatika wafanyabiashara wilayani hapa wameshauliwa kuitumia taasisi ya biashara,viwanda na kilimo Tanzania TCCIA ili kupata ushauri wa kibiashara na kuondokana na migogoro.

Wito huu unakuja kufuati kuwepo kwa mgomo wa wafanyabiashara katika soko kuu la kyela kwa madai ya kuwepo unyanyasaji kutoka mamlaka ya mapato Tanzania TRA tawi la kyela kuwakamata wateja wanaonunua bidhaa sokoni hapo na kudai risiti kuwa ni kinyume cha utaratibu.

Akizungumza mara baada ya kutamatika kwa mgogoro huo mwenyekiti wa taasisi ya biashara,viwanda na kilimo Tanzania TCCIA wilaya ya kyela CPA Dony Koroso amesema,moja ya kazi ya taasisi hiyo ni kuwahudumia wanachama   katika kutatua migogoro na kuwatafutia masoko ambapo bado hawafungwi kutoa ushauri kwa wafanyabiashara nje ya wanachama.

Sauti ya Koroso kuhusu ushauri

Koroso ameongeza kuwa,migogoro mingi inayotokea kati ya mamlaka ya mapato Tanzania TRA na wafanyabiashara, ni kukosekana elimu kwa baadhi ya wafanyabishara na kuona kuna uonevu kutoka mamlaka hiyo,ambapo amesema TCCIA   imekuwa ikiwatumia wataalamu katika kushuhghulikia migogoro.

Sauti ya Koroso kuhusu kutatua mgogoro

Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa TCCIA amesema mgomo wa wafanyabiashara ambao umetokea hivi karibuni na kupelekea huduma za maduka kukosekana kwa siku tatu umechagizwa zaidi na masula ya kisiasa ndani yake.

Sauti ya koroso kuhusu mgomo

Koroso amemaliza kwa kutoa rai kwa viongozi wa chama cha mapinduzi ccm ambao ndiyo wamiliki wa soko hilo kuajiri Mkuu wa soko ambaye atasimamia shughuli  zote za soko na kutoa taarifa kwenye uongozi wa ccm,tofauti na ilivyo sasa ambapo wapo viongozi wa soko wanaosimamia na kuamua mambo yanayoweza kuleta athari mbaya kwa chama cha mapinduzi.

Sauti ya koroso ushauri kwa chama cha mapinduzi ccm ambao ndiyo wamiliki kuhusu soko kuu la kyela

Taasisi ya wafanyabiashara,viwanda na kilimo Tanzania TCCIA ilianzishwa mwaka 1988 kwa msaada wa Serikali ya Tanzania ili kuimarisha sekta binafsi.