Pichani katibu wa Ccm wilaya ya Kyela Amosi Kusakula akiwa na wajumbe wa chamata mkoa wa mbeya wilayani Kyela wakati wa zoezi la utambulisho katika ofisi za ccm wilaya ya Kyela Picha na Elizabeth Asajile
Katika kuhakikisha kuwa kero za wananchi wilayani kyela zinatatuliwa ipasavyo na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania chini rasisi Samia Suluhu Hasani taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya CHAMATA TANZANIA imetakiwa kuibua kero za wananchi waishio vijijini.
Na James Mwakyembe
Uongozi wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya CHAMATA TANZANIA umefika na kujitambulisha rasmi kwa vyombo vya kiserikali tayari kuanza majukumu ya kumsemea rais Samia Suluhu Hasan jamii ya kitanzania.
Ujumbe huo ukiongozwa na mwenyekiti Wiliam Mwangomile na Katibu Imani Mwambusye ambao ni viongozi wa CHAMATA TANZANIA wilaya ya Kyela umefika katika ofisi za Ccm wilaya ya Kyela,Ofisi ya Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela,ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na kituo cha polisi wilaya ya Kyela.
Akizungumza mara baada ya kupokea ugeni wa chamata wilaya ya Kyela katibu wa chama cha Mapinduzi wilaya Amosi Kusakula ameipongeza taasisi hiyo kwa kuamaua kulibeba jambo hilo ambalo amekiri kuwa lilipaswa kufanywa na chama cha mapinduzi wao wenyewe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao ya kichama
Kadharika Kusakula ametoa Baraka zote kwa taasisi hiyo na kuahidi kuwa nao bega kwa bega katika kila jambo huku akiitaka taasisi hiyo kuibua changamoto za watanzania kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Kyela hususani vijijini ili serikali na chama waweze kuzitatua changamoto hizo.
Kwa upande wake katibu mtendaji wa CHAMATA TANZANIA Wilaya ya Kyela Imani Mwambusye amemshukuru katibu huyo wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kyela pamoja na taasisi zingine walizozifikia ambapo amewataka watanzania wengine walio na mapenzi mema na raisi Samia Suluhu Hasan kujiunga na CHAMATA TANZANIA na kupuuza uvumi wa baadhi ya watu wanaodai taasisi hiyo haijasajiriwa kisheria.
Sauti ya katibu wa CHAMATA TANZANIA Imani Mwambusye akizungumzia kuhusu pongezi zake kwa taasisi walizozifikia katika utambulisho
Taaisisi ya CHAMATA TANZANIA ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo kazi yake kubwa ni kumsemea Mama Samia Suluh hasani kwa watanzania juu ya kazi zake anazozifanya na kuzifikisha sawasawa na malengo mahususi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwa nchi yetu ya Tanzania.