Kyela:Wanafunzi zaidi ya 40 hawajaripoti Ngonga Sekondari
30 January 2024, 22:16
Wakati mhura mpya wa masomo ukianza rasmi hapa nchini Tanzania zaidi ya wanafunzi 40 hawajaripoti katika shule ya sekondari Ngonga kutokana na sababu zisizotambulika na mamlaka husika.
Na Nsangatii Mwakipesile
Mtendaji wa kata ya Ngonga Lutufyo Mwangamilo ametoa tahadhari ya magonjwa ya mlipuko ikiwamo kipindupindu kwa wakazi wa kata ya ngonga hapa wilayani Kyela kwa kujenga vyoo bora vilivyo na maji tiririka pamoja na kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa hayo hatari.
Mtendaji wa kata ya Ngonga Lutufyo Mwangamilo amewaomba wananchi wa kata hiyo kuakikisha wanajikinga na mambukizi ya ungonjwa hatari wa kipindupindu.
Akizungumza na Keifo Fm Mwangamilo amewatahadharisha wananchi wa kata hiyo kwa kuhakikisha wanazingatia kanuni zote za usafi wa mazingira ikiwemo ujenzi wa vyoo bora vilivyo na maji tiririka hali itakayowakinga na magonjwa ya mlipuko ikiwamo kipindipindu.
Katika hatua nyingine Mwangamilo ametoa taarifa juu ya wanafunzi waliofauru na kuripoti katika shule ya sekondari ya Ngonga ambapo amesema jumla ya wanafunzi miamoja na therasini wameripoti na wengine zaidi ya arobaini hawajaripoti shuleni hapo.
Kuhusu wanafunzi ambao hawajaripoti mtendaji huyo amesema serikali haitalifumbia macho jambo hilo hivyo kuwataka wazazi wa watoto ambao hawajaripoti kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni haraka kabla mkono wa sheria haujawafikia.
Msimu mpya wa masomo kwa mwaka 2024 umezindiliwa rasmi tarehe 8 Januari 2024 ambapo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wameanza masomoa yao mapya kwa mwaka husika ikiashiria mwaka mpya wa masomo katika tasnia ya elimu Tanzania.