Kyela:CHAMATA Kyela wakiwasha
30 January 2024, 22:07
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya CHAMATA Tanzania wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya wameafikiana kuanza kufanya shughuli za utambulisho wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani.
Na James Mwakyembe
Kikao kazi cha kujadiri kuiimarisha CHAMATA wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya kimefanyika huku wajumbe wa kikao hicho wakiridhia kwa pamoja juu mambo mbalimbali ya kuimarisha taasisi hiyo mpya ndani ya wilaya ya Kyela.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na mwenyekiti wa Chamata Wilaya ya Kyela Wilium Mwangomile wajumbe wamejadiri hoja mbalimbali zilizolenga kumtangaza na kumsemea Mama Samia Suluhu Hasani Raisi wa jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anazozifanya kwa watanzaia.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi hicho Adamu Mwandali,Upendo Mwandali na George Aldoltego miongoni wa wajumbe wa CHAMATA wilaya ya Kyela wamesema wamekoshwa na kazi kubwa anazoendelea kuzifanya Mama Samia Suluhu Hasani hivyo haoni sababu ya kushindwa kuyasema mazuri mbele ya watanzania wachache wasiojua kuhusu mazuri hayo.
Kwa upande wa mwenyekiti wa CHAMATA Kyela Wiliam Mwangomile amewashukuru wajumbe kwa kushiriki kikamirifunkatika kikao hicho na kuwaomba watanzania kuhakikisha katika kikao kijacho wanavunja rekodi ya mikoa Mingine pamoja na kutambulisha shughuli mbalimbali za kijamii zinazotaraijiwa kufanyika katika siku chache zijazo.
CHAMATA ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali iliyosajiriwa na mamlaka husika ambayo kazi yake kubwa ni kuhakikisha wanamsemea mazuri anayoyafanya Mama Samia Suluhu Hasani kwa watanzania wachache wasiojua baada ya kuwepo kwa upotoshaji wa baadhi wa wanasiasa wasiopenda maendeleo ya Tanzania ya awamu ya sita chini ya Rais Kipenzi cha watu Samia Suluhu Hasani.
Samia Mitano tena ni lazima