Kyela: Mwamengo, UWT Nkuyu watoa kilo mia moja za mchele
27 January 2024, 00:30
Wakati Jumiya ya UWT kata ya Nkuyu ikijiandaa kusherehekea sikukuu yao, kilo miamoja za mchele zimetolewa na mdau wa maendeleo hapa wilayani Kyela Baraka Mwamengo.
Na James Mwakyembe
Kuelekea sherehe za jumuiya ya umoja wa wanawake UWT kata ya Nkuyu mdau wa maendeleo na mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Basai General Supply Ltd Baraka Mwamengo ametoa kilo miamoja za mchele ili kufanikisha sherehe hizo.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi huyo afisa miradi wa Basai General Supply Ltd Antony Mwamkonda amesema siku chache zilizopita alipokea barua ya ombi la kina mama hao ambapo kulingana na taratibu walizojiwekea waliona vema kushiriki kikamirifu katika hafra hiyo kwa kutoa kilo mia moja za mchele.
Kadharika Mwamkonda ameongeza kuwa wao kama kampuni ya ujenzi imekuwa ni wajibu wao kushirikiana na jamii ya wanakyela hasa kwa kurudisha nyumbani kiasi cha asilimia kumi katika kila kazi wanazozifanya hapa wilayani kyela kisha kazidi kufungua milango kwa wahitaji.
Kwa upande wa diwani wa kata ya Nkuyu Hezron Mwalusangani amemshukuru Baraka Mwamengo kwa mchango wake huo na kuendelea kumsihi kuisaidia kata yake katika mambo kadha wa kadha ya kimaendeleo katika kata hiyo
Wakitoa neno la shukrani kwa niaba ya kina mama wengine wanaunda jumuiya ya wanawake UWT kata ya Nkuyu katibu wa jumuiya hiyo Kisa Fungo na Zubeda Ndimbo wamemshukuru mdau huyo kwa utii mkubwa wa kuwakumbuka kuwapatia kilo hizo mia moja za mchele katika siku yao hiyo muhimu.
Basai General Supply Lmt ni kampuni ya kizawa iliyochini ya mkurugenzi Baraka Ulimboka Mwamengo ambayo imekuwa ikifanya kazi mbalimbali za kimaendeleo katika wilaya ya Kyela ikiwemo ujenzi wa Barabara unaoendelea katika maeneo mengi hapa wilayani.