Kyela: Aliyeshinda rufaa ya kifungo cha maisha achukua fomu kugombea BAVICHA
21 December 2023, 13:22
Mshindi wa rufaa ya kifungo cha maisha Gerald Mwakitalu amechukua fomu ya kugombea nafasi ya mwenyekiti wa Balaza la Vijana Chadema BAVICHA wilaya ya Kyela na kuwaomba wajumbe kumchagua.
Na James Mwakyembe
Wakati uchaguzi wa ndani kwa ngazi ya wilaya ukipigwa kalenda hapa wilayani Kyela mgombea wa nafasi wa mwenyekiti BAVICHA wilaya Gerald Mwakitalu amewaomba wapiga kura kumchagua yeye ili kukijenga chama katika sura mpya.
Amesema hayo muda mfupi baada ya zoezi la usahiri kukamilika na msimamizi wa uchaguzi kupitia chama hicho kutangaza kuahirisha mpaka januari 1 2024 baada ya baadhi ya kata kutokamirisha uchagauzi wao.
Amesema ameamua kuingia katika kiny’ang’any’iro hicho ili kutoa mchango wake kwa ngazi ya wilaya ili kuwaunganisha vijana wa chama hicho pamoja na wasio wanachama.
Mwakitalu amewaomba wapiga kura kutofanya makosa katika kumchagua mtu makini mwenye maono ya kuiunganisha BAVICHA kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na ule mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025.
Kadharika Mwakitalu amewataka wapinzani wake kwenye nafasi hiyo kwa ngazi ya wilaya kughairisha mpango wao wa kugombea nafasi hiyo kwani yeye anajitosheleza hivyo hakuna sababu ya wao kuingia na kushindana naye hivyo kuwataka kumpa kura zao zote pamoja na wapiga kura wao.
Uchaguzi wa ndani wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wilaya ya kyela umeahirishwa mpaka January 5 2025 baada ya ule wa kwanza kushindwa kufanyika kutokana na baadhi ya kata kutofanya chaguzi zao.