Mwinuka: Asante serikali Mwangany’anga imekuwa jicho la Kyela
13 December 2023, 16:48
Diwani wa kata ya Mwangany’anga wilayani Kyela Alex Mwinuka ameishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa ujenzi wa kipande cha barabara kinachojengwa kwa kiwango cha lami katika kata hiyo.
Na Nsangatii Mwakipesile.
Wakati serikali ikiendelea na jitihada za kuwaletea wananchi wake maendeleo hapa nchini Tanzania diwani wa kata ya Mwangany’anga Alex Mwinuka ameishukuru serikali ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania ikiongozwa na Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo aliyo waletea ndani ya kata hiyo.
Akizungumza na Mwandishi wa habari Mwinuka amesema mpaka sasa serikali kupitia mamalaka zake wameendelea kutekeleza miradi mbalimbali katika kata hiyo ambayo ni ujenzi wa barabara ya Kyela sekondari kuelekea mamlaka ya mji mdogo wa Kyela unaogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni miatatu,Ujenzi wa madaraja madogo matatu maarufu kama karavati jambo ambalo amelitaja kuwa mwalobaini kwa wafanyabiashara wa soko la Olofea na wananchi kwa ujumla.
Kwa upande wa miundombinu ya Elimu katika kata ya Mwangany’anga Mwinuka amesema serikali imepeleka jumla ya shilingi milioni hamsini na tano kwaajiri ya ujenzi wa vyoo matundu matatu ya kisasa katika shule ya sekondari ya kutwa ya Kyela inayopatikana kwenye kata hiyo pamoja na kujenga madarasa mawili katika shule ya msingi Uhuru na Mbugani.
Kuhusu ujenzi wa Zahanati amesema wanakusudia kujenga zahanati kwa nguvu za wananchi pamoja na kubainisha kuwa mpaka sasa wamekwisha wasiliana na mamlaka ya mji mdogo ili waweze kuwapatia moja kati ya maeneo yanayopatikana ndani ya kata hiyo ili ujenzi uanze.
Kata ya Mwangany’anga ni miongoni mwa kata zinazopatikana hapa wilayani Kyela ambazo zimekuwa zikikabiriwa na kadhia kubwa ya miundombinu mbalimbali chakavu hivyo kwa jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini Raisi Samia Suluhu Hasani zinaonesha dhamira ya dhati ya kuwainua wananchi ndai ya kata hiyo kongwe hapa wilayani Kyela.