Mwankenja: CHADEMA tulieni mambo mazuri yanakuja
11 December 2023, 12:31
Uchaguzi wa ndani wa chama cha demokrasia na amaendeleo CHADEMA ngazi ya kata ya Kyela mjini umefanyika na kumpata Lafaele Mwankenja kuwa menyekiti.
Na James Mwakyembe.
Zoezi la uchaguzi wa ndani kuchagua viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA limendelea hapa wilayani Kyela mkoani Mbeya ambapo Mwenyekiti wa uchaguzi Prospa Mwakilembe washukuru wanachama wa chama hicho kwa utulivu na kufanikisha uchaguzi kwa amani na upendo.
Akizungumza na mwandishi wa habari Mwakilembe akiwa ofisi za chama cha demokrasia maendeleo CHADEMA zilizopo kata ya Kyela mjini amesema tangu kuanza kwa zoezi hilo kuanza katika kata hiyo wanachama wamejitokeza kugombea nafasi mbali mbali ambapo hatua za kuwapata viongozi kupitia kata zimefanyika.
Amesema baada ya hutua hizo tayari viongozi wa ngazi ya kata wamepatikana ambao ni Lafaeli Mwankenjaaliyechaguliwa kwa nagazi ya amwenyekiti na katibu wake ni Evance Mwakasege huku katika nafasi ya uenezi aliyechaguliwa ni Timoth Luvanda.
Mshindi wa nafasi ya uenezi kwa ngazi ya kata ya Kyela mjini Timoth Luvanda amewashurukuru wapiga kura wote na kuahidi kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja na kukieneza chama hicho kwa wananchi wote wa kata ya akyela na wilaya kwa ujumla.
Akizungumzia ushindi alioupata mwenyekiti mpya ndani ya kata ya Kyela mjini Lafaele Mwankenja yeye amewashukuru na kuwataka wananchama wa kata hiyo kudumisha mshikamano hasa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na kuungana katika uchaguzi mkuu ujao.
Uchaguzi wa ndani wa chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA unatarajia kuendelea tena kwa ngazi ya wilaya hapo kesho katika kiny’ang’anyiro kinachotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa nafasi ya mwenyekiti wa wilaya ya Kyela.