Keifo FM

Wananchi Kyela wakimbia nyumba zao kwa harufu ya mizoga

6 December 2023, 18:06

Picha ya Kizimba cha roma kikiwa kimejaa taka zinazosababisha kero kubwa kwa wakaazi wa kitongoji hicho.Picha Na James Mwakyembe

Wakaazi wa kitongoji cha roma wanaokizunguka kizimba cha Roma wameitaka serikali ya mamlaka ya mji mdogo wa Kyela kuziondoa taka zinazozagaa katika kizimba hicho ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko.

Na Nsangatii Mwakipesile

Kufuatia kuwepo kwa kadhia ya harufu mbaya inayotakana na taka kuoza bila kuondolewa kwa wakati katika kizimba kilichopo uwanja wa mchaga hapa wilayani kyela wananchi wa kitongoji cha roma kata ya Mbungani wamelalamikia kero hiyo na kuitaka serikali kuondoa taka hizo.

Wakizungumza na keifo fm wananchi hao wakiwa karibu kabisa na kizimba hicho wamesema kizimba hicho kimekuwa kero kwa watoto na hata watu wazima kutokana na taka zinazotupwa hapo kuwa hatarishi kwa afya hali inayotishia kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.

Sauti ya Felista Leifosi akizumzia kadhia ya kizimba cha roma

Katika hatua nyingine nyingine mkazi wa kitongoji hicho Felista Laifosi amesema wamekuwa wakikutana na kadhia kubwa ya harufu mbaya ya mizoga inayotupwa ka Nguruwe,Ng’ombe na Mbwa na mizoga mingine hali inayowanyima uhuru wa kukaa katika maeneo yao.

Sauti ya Feilista Leifosi akizungumzia kadhia ya mizoga kizmbani hapo

Pamoja na hayo keifo fm ilifunga safari kumtafuta mwenyekiti wa kitongoji cha Roma Maiko Mwakibinga na kuzungumza naye kufuatia kadhia hiyo ambapo Mwakibinga amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kusema kuwa yeye kama kiongozi amekuwa akiwasiliana mara kwa mara na viongozi wa Mamlaka ya mji mdogo Kyela ili kuleta gari kuziondoa taka hizo licha ya kukiri kuwa gari hiyo imekuwa ikielemewa.

Sauti ya Michael Mwakibinga mwenyekiti wa kitongoji cha roma kuhusu kukiri kuzidiwa
Picha Mwenyekiti wa Kitongoji cha roma Michael Mwakibinga akiwa ofisini kwake.

Pamoja na hayo amewaomba wananchi wanao tumia kizimba hicho kuzingatia matumizi sahihi ya kuzihifadhi taka kizimbani hapo na kukemea vikari uwepo wa baadhi ya wananchi wanaotupa taka nje ya kizmba hicho.

Sauti ya Michael Mwakibinga mwenyekiti wa roma kuhusu elimu

Amehitimisha kwa kuishukuru mamlaka ya mji mdogo wa Kyela kwa kuzingatia utoaji wa gari ya kuzoa taka katika eneo la mamlaka ya mji mdogo na kuendelea kuwaomba kujitahidi kufika mara kwa mara kitongojini humo hasa kwenye kizimba hicho ili kufanya mazingira kuwa safi na salama kwa wananchi wanaozunguka kizimba hicho.