Bongo: Mkurugenzi mpya apewe maua yake
4 December 2023, 12:33
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela Emmanuely Bongo amewataka wenyeviti wa vitongoji na mitaa kuhakikisha wanazingatia suala la utawala bora ili kuwaletea wananchi maendeleo.
Na Nsangatii Mwakipesile
Kikao cha Robo ya kwanza cha Mamlaka ya mji mdogo wa Kyela kimefanyika na wakijadili ajenda mbambali zilizowasilishwa mbele ya baraza hilo katika ukumbi wa mikutano wa Komyuniti Senta.
Akizungumza katika kiako hicho mwenyekiti wa baraza la mamlaka ya mji mdogo wa Kyela Emmanuely Kharison Bongo amewataka wenyeviti wa vitongoji hapa wilayani kyela kuhakikisha wanafanya mikutano na kusoma mapato na matumizi mbele ya wananchi.
Kuhusu makusanyo ya mamlaka ya hiyo Bongo ameeleza kuwa mpaka sasa wamekusanya jumla ya shilingi milioni mia nne sabini na mbili mia sita sabini na saba mia tisa na tano na senti sabini nan ne ya makisi ya fedha ya bajeti ya fedha kwa mwaka 2022-2023 ambazo zilikuwa ni shilingi milioni mia tano ishirini na hamsini na moja elfu.
Kadharika Bongo amesema mamlaka hiyo imeendelea kukamirisha miradi mbalimbali ya maendeleo inayopatikana katika kata za Ndandalo,Nkuyu,Bondeni na Kyela mjini huku mamlaka hiyo ikitenga jumla ya shilingi milioni ishirini kwaajiri ya kununua eneo la kutunza taka ngumu.
Ametumia muda huo kuwakumbusha viongozi hao wa mitaa kuhakikisha wanawakumbusha na kuwahimiza wazazi kuhusu kuwapeleka watoto wote walio na umri wa kwenda shule pamoja kuwakumbusha wananchi juu ya kilimo katika msimu mpya.
Amehitimisha kwa kumshukuru mkuu wa wilaya ya Kyela na ofisi ya mkurugenzi na watalaamu kwa ujumla kwa namna anavyotoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo ya mji mdogo hali inayopelekea maendeleo ya wilaya kukua kwa haraka.