Kyela walia na mkandarasi wa mradi wa umwagiliaji Makwale
28 November 2023, 11:49
Baada ya kushindwa kukamilika kwa wakati kwa mradi wa umwagiliaji wa Makwale hapa wilayani Kyela wananchi wanaunda kata za Makwle,Ndobo na Lusungo wameiomba serikali ya halmaashsuri ya wilaya ya kyela kuingilia kati kukamilika kwa mradi huo.Na Nsangatii Mwakipesile
Kutokana na kusuasua kukamilika kwa mradi wa kilimo cha umwagiliaji wa Makwele uliopo hapa wilayani Kyela, Diwani wa kata ya Ndobo Ambakisye Njelekela ameiomba serikali kuingilia kati kutatua mkwamo huo.
Haya yanajiri ikiwa ni miezi miwili tangu mradi huo mkubwa kuzinduliwa kiongozi wa mbio za Mwenge kitafa Abdalla Shaib Kaim ukiwa namatumaini rukuki ya kuinua uchumi kwa wananchi wa kata za Makwale, Ndobo, Lusungo na Mababu.
Akizungumza na mwandishi wa kituo cha Keifo Fm Nsangatii Mwakipesile Diwani huyo amesema wananchi wa kata yake hambao ni sehemu ya wanufaika wa mradi huo ambao walijawa na matumaini ya kunufaika nao sasa wamekata tamaa kutokana na kuchelewa kuanza kufanyakazi.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo amemuomba mkuu wa mkoa wa mbeya Juma Homera na mkuu wa wilaya ya Kyela Josephine Manase kumhimiza mkandarasi wa mradi huo kuumaliza kwa wakati ili uanze kunufaisha wananchi wa Kyela.
Mradi wa umwagiliaji wa Makwale ni miongoni mwa Miradi iliyofunguliwa na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu Abdalla Shaibu Kaim mnamo mwezi septemba mwaka huu.