Serikali ya Mwaga Boti nne za kisasa kwa wavuvi ndani ya ziwa Nyasa
28 November 2023, 11:28
Naibu waziri wa Kilimo na Uvuvi Alexander Mnyeti amewataka wavuvi ndani ya Ziwa Nyasa kuhakikisha wanaachana na uvuvi haramu na badara yake watumie uvuvi wa vichanja ili kukuza uchumi wa Taifa.Nsangatii Mwakipesile
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi hapa nchini Tanzania Alexander Pastory Mnyeti amefanya ziara ya kikazi katika wilaya ya Kyela mkoani Mbeya na kukabidhi boti nne za kisasa kwa wavuvi kwa mikoa ya Mbeya,Njombe na Ruvuma katika bandari ya Kiwira.
Akizungumza akiwa katika Bandari ya kiwira wilayani kyela Mnyeti amemshukuru raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hasani kwa kuzitoa boti hizo kwa wavuvi ndani ya ziwa Nyasa huku akiwataka kuhakikisha wanazingatia mikataba ili waweze kunufaika na misaada hiyo.
Katika hatua nyingine Mnyeti amesema lengo la Raisi ni kuhakikisha anaifufua sekta ya Uvuvi ambapo zoezi hilo lililanzia Rufiji na kisha mkoani Tanga na kisha kwa mikoa ya Mbeya,Njombe na Ruvuma na baadae katika mikoa ya Rukwa na Kigoma ambapo jumla ya boti 166 zimetolewa na Raisi kwa awamu hii ya kwanza.
Kuhusu ujenzi wa Taifa Mnyeti amewapongeza wakuu wa mikoa ya Mbeya,Njombe na Ruvuma kwa namna wanavyoshiriki kikamirifu katika kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuhakikisha uchumi unasonga mbele wa wananchi wa Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya wanufaika wa mikopo hiyo Mkurugenzi wa Asasi ya Kyela Education Improvement Foundation Gabiel Martin Kipija amemshukuru rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuwapatia mopo huo ambao amekiri kuwa unafungua fursa nyingi kwa vijana waliokosa ajira katika mkoa wetu wa Mbeya.
Mikopo hiyo imetolewa na raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia suluh Hasani kupitia Bank ya Kilimo Tanzania Agriculture Development Bank TADB lengo likiwa ni kuifufua sekta ya Uvuvi ambayo inatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kufungua fursa ya ajira kwa watanzania.