Wananchi Kyela washauriwa kuachana na imani potofu zoezi la utoaji chanjo kwa watoto
21 September 2023, 13:27
Wakati zoezi la utoaji chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka 8 likianza hii leo wazazi na walezi wilayani Kyela wameaswa kuachana na imani potofu, bali wanatakiwa kuamini chanjo inayotolewa na watoa huduma waliowekwa na serikali.
Na Secilia Mkini
Katika kuhakikisha zoezi la chanjo ya polio linafanikiwa, wananchi wilayani Kyela wameaswa kutoa uishirikiano kwa serikali ili watoto waweze kupata chano hiyo.
Haya yamejiri wakati wa kampeni ya utoaji elimu kwa jamii kupitia watoa huduma ya afya kwa jamii ambao wamewaasa wananchi kuepukana na imani potofu juu ya chanjo hizo na badala yake kila mzazi mwenye mtoto ahakikishe kuwa mwanae anapata chanjo hiyo .
Katika hatua nyingine wameeleza namna wanavyowafikia wanajamii ili kuwapatia elimu ikiwemo katika shughuli mbalimabali za kijamii kama sherehe na maafa.
Kwa upande wake katibu wa watoa huduma ya afya ngazi ya jamii Bakari Samson amewaasa wazazi na walezi kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa serikali ili kufikia malengo yaliyopangwa na serikali .