Kinanasi: Yajayo Kyela yanafurahisha
14 September 2023, 19:21
Mbunge wa Jimbo la Kyela Ally Mlagila Jumbe Kinanasi ameahidi kutekeleza mambo yote yaliyoombwa na wananchi wa kata ya Bujonde ikiwemo barabara ya kutoka Bujonde kwenda Nyerere ndani ya kata hiyo.
Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi katika kata hiyo huku akiwaasa wananchi kuongeza ushirikiano kwa ajili ya maendeleo binafsi na taifa kwa ujumla.
Aidha Kinanasi amewatoa hofu wananchi wa kata hiyo juu ya suala la bei ya kokoa kwani ni adha iliyowakumba kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Kinanasi amewapongeza wananchi wa jimbo la Kyela kwa kuwa na umoja licha ya utofauti wa kivyama na tofauti nyinginezo.
Aidha mbunge Kinanasi amewashukuru wananchi kwa kujitokeza katika ziara hiyo ambayo ilihusisha uzinduzi wa madaraja mawili ya kata hiyo yaliyojengwa na wananchi wa kata ya Bujonde.