Kuvunjika kwa ndoa chatajwa kuwa chanzo cha wimbi kubwa la watoto mitaani
12 September 2023, 12:31
Uwepo wa migogoro mingi baina ya wanandoa imepelekea ndoa nyingi kuvunjika imetajwa kuwa ni sababu kubwa inayo sababisha uwepo wa watoto wa mitaani ambao wanakosa kuwa na makazi maalumu.
Na mwandishi wetu james mwakyembe
Kuvunjika kwa ndoa, malezi duni pamoja na misukosuko ya mahusiano imetajwa kuwa sababu kubwa inayo pelekea wimbi kubwa la watoto wasio na maadili mema na wengine kuwa wezi kulingana na watoto hao kukosa malezi bora kutoka kwa wazazi.
Kauli hiyo imetolewa na Justin Sailasi afisa ustawi wa jamii wilayani kyela ambapo amesema watu wengi wanaingia katika mahusiano kwa mihemuko hatua inayo pelekea ndoa nyingi kuvunjika na kuwaacha watoto wakiapata tabu.
Amesema watoto wengi wanaogeuka kuwa wezi ni wale wanao pambana kupata chochote kitu ili weweze kukizi mahitaji yao ya masingi kama vile chakula.
Mapema nimefika ofsini kwa justini sailas afisa utsawi wa jamii hapa wilaya kyela kwanza nimetaka kujua wimbi hili la watoto wengi kugeuka kuwa wezi linatokana na nini?