Wadau wajipanga kukomesha utapiamlo Kagera
20 December 2024, 10:58 am
Utapiamlo ni hali mbaya ya lishe ambayo inaweza kuwa pungufu au iliyozidi. Katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, utapiamlo ulioenea zaidi ni ule wa ulaji duni.
Na Jovinus Ezekiel
Wadau wa lishe mkoani Kagera wametakiwa kuwa mstari wa mbele kushirikiana na serikali kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora katika jamii kwa lengo la kupunguza hali ya utapiamulo mkoani Kagera.
Akizungumuza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kikao cha mawasilisho ya bajeti za lishe kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika mjini Kayanga wilayani Karagwe kwa kujumuisha wadau mbalimbali wa lishe ,Afisa lishe wa mkoa wa Kagera Joanitha Jovin amesema kuwa ni muda muafaka kwa wadau wa lishe mkoa wa Kagera kuendelea kushirikiana na serikali ili mkoa wa Kagera uondokane na changamoto ya udumavu.
Amesema kuwa kwa bajeti ya lishe ya mwaka wa fedha 2025/2026 miongoni mwa vipaumbele ambavyo vimependekezwa na wadau kutekelezwa kwa kushirikisha maafisa mipango ni kuhakikisha elimu ya lishe inatolewa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma za kutolea lishe zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikoa hicho Beatirice Laurent afisa afya wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe amesema kuwa kutokana na elimu ya lishe inayozidi kutolewa jamii inazidi kujua umuhimu wake na ikizidi kutolewa wananchi watajua umuhimu wa kutumia vyakula vyenye lishe