Karagwe FM

Miaka 16 ya askofu Rweyongeza yazaa parokia 9 na mapadre 32

7 November 2024, 9:56 pm

Mwenye kofia ni Askofu wa Jimbo Katholiki la Kayanga Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza. Picha na Ospicia Didace

Jimbo Katholiki la Kayanga lililozaliwa kutokana na jimbo Katoliki la Rulenge Ngara limetimiza miaka 16 kwa mafanikio makubwa ikiwemo ongezeko la Parokia na mabadiliko makubwa ya kimazingira.

Na Ospicia Didace

Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza ameadhimisha miaka 16 ya uaskofu na kuanzishwa kwa jimbo hilo akijivunia mafanikio makubwa yaliyofikiwa ikiwa ni pamoja n ongezeko la Parokia kutoka 11 hadi parokia 20, kupadirisha madre 32 sambamba na kuwepo kwa ongezeko la mafratel wanaotajia kuwa mapadre hapo baadaye.

Mhasham Askofu Rweyongeza amesema hayo Novemba 6 .2024 katika kanisa kuu la Mtakatifu George Jimbo Katholiki la Kayanga wakati wa misa takatifu ya shukurani ikiadhimishwa miaka 16 ya jimbo Katholiki la Kayanga na miaka 16 ya uaskofu wake.

Sauti ya askofu Almachius Rweyongeza wa jimbo Katholiki la Kayanga
Askofu Rweyongeza akibariki miche ya miti kabla ya kuigawa kwa mapadre na baadhi ya viongozi wa kanisa Katholiki jimbo la Kayanga. Picha na Ospicia Didace

Askofu Rweyongeza ambaye amejipambanua kama rafiki wa mazingira ameendelea kuwasisitiza waumini na viongozi wa kanisa wakiwemo mapadre kupanda miti ili kuendelea kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi huku akiahidi kuwagawia mapadre miche ya miti aina ya mipodo wakapande katika parokia zao

Sauti ya Askofu Rweyongeza akiongelea umuhimu wa kutunza mazingira kwa kupanda miti